Yesu mpendwa
Nahisi ni kama mimi ni yatima kwa matrix,kwa jamii iliyo baridi mioyoni na iliyo mbali na wewe…nisaidie nitoke humo.

nahisi kama yatima kwa kanisa yangu,mi bikira ndio lakini nimelala…nisaidie nikajiamshe mwanzo na kabisa.

najihisi kama yatima ingawa masauti ya manabii uliyotuma kitambo na zama za zama…nisaiddie nisikie sauti yako leo kwa ukubwa na wazi.

najihisi ni kama nimekua yatima kutoka utajiri ajabu wa tabia yako na maadili…nisaidie nikanunue dhahabu kutoka kwako,

nahisi kama yatima kwa upendo wako…nisaidie kwa kujaza moyo wangu na joto la upendo.

nahisi yatima kwa nyumbani mbinguni na kwa baba yangu MOLA…rudi haraka tafadhali eh Yesu!

Yesu,wacha wafuasi wako walio kwa matrix wasikie sauti yako tena…tuma roho wako wa unabii…tutumie nabii aliye na roho na nguvu za eliyah vile tu uliahidi kupitia mtumwa wako malakia 4:5.mtumishi wako atakaye badilisha mioyo ya watoto kuelekea baba zao vile uliahidi kwa mathayo 17:11 na hii,itarudisha vitu vyote upya na kuweka picha yako kwa wafuasi wako.

mwana wako na mfuasi na mwanachama wa kanisa yako