Duniani kumejaa makanisa, madhehebu, makundi, na imani tofauti. Swali laibuka: Mbona Christian Style? si hili swala laendelea kujaza barabara ya kidini na kiroho ambayo keshajaa? na kuleta utata kwa mwanadamu anayeendelea kutafuta ukweli na maana halisi ya maisha?
Miaka elfu mbili iliyopita wakati wa Kristo, watu wengi waligeukia wafuasi wa Yesu kuwaomba wamwone Yesu binafsi. Hili lilikuwa ombi rahisi kwa maneno machache mno, pia hili ombi lilionyesha hitaji la ndani la mwanadamu kumwona Yesu.
Tamanio ambalo mwanadamu ameliweka rohoni kwa muda mrefu. Ndio hata leo wakaaji wa Matrix kwa hitaji kuu huwaomba wafuasi wa Yesu wawaonyeshe Huyu Yesu maarufu.
Hakuna swali laweza kuwakilisha matrix ya leo, siku za mateso, uchungu na kupoteza tumaini .
Ombi hili linawasilisha nafasi maalum kwa wafuasi wa Yesu, na kwa wakati huo huo kuficha tishio kubwa: kutowaonyesha Matrix kuhusu Yesu ni kama kutangaza kifo cha Ukristo. Huu ndo wakati mwafaka wa kuwaonyesha Yesu, tabia yake ya upendo, kwao Matrix na kwa sayari yote ya dunia, na kama mfuasi wa Yesu, nina nafasi ya kuwafanya wana Matrix kuigusa mbingu kwa vidole vyao. kutayarisha njia kwa Kristo anayetaka kunipeleka nyumbani mwishowe.